Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. 2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. 3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. 4 Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. 5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki. 6 Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
SIRI ZA BIBLIA
Отметить все как (не)прослушанные ...
Manage series 3273506
Контент предоставлен SIRI ZA BIBLIA. Весь контент подкастов, включая эпизоды, графику и описания подкастов, загружается и предоставляется непосредственно компанией SIRI ZA BIBLIA или ее партнером по платформе подкастов. Если вы считаете, что кто-то использует вашу работу, защищенную авторским правом, без вашего разрешения, вы можете выполнить процедуру, описанную здесь https://ru.player.fm/legal.
Maarifa ya ki-Mungu na namna ya kuliishi kusudi lako
…
continue reading
119 эпизодов