Player FM - Internet Radio Done Right
Checked 11M ago
Добавлено три года назад
Контент предоставлен SIRI ZA BIBLIA. Весь контент подкастов, включая эпизоды, графику и описания подкастов, загружается и предоставляется непосредственно компанией SIRI ZA BIBLIA или ее партнером по платформе подкастов. Если вы считаете, что кто-то использует вашу работу, защищенную авторским правом, без вашего разрешения, вы можете выполнить процедуру, описанную здесь https://ru.player.fm/legal.
Player FM - приложение для подкастов
Работайте офлайн с приложением Player FM !
Работайте офлайн с приложением Player FM !
Подкасты, которые стоит послушать
РЕКЛАМА
Sometimes a place we consider quiet is just a place we haven’t taken the time to listen. Threshold is nonprofit, listener-supported, and independently produced. You can support Threshold by donating today . To stay connected, sign up for our newsletter . We want to hear from you! Send us your questions about the new season, the content or how it’s made, for an upcoming behind-the-scenes episode. You can submit your questions to outreach@thresholdpodcast.org…
SIRI ZA BIBLIA
Отметить все как (не)прослушанные ...
Manage series 3273506
Контент предоставлен SIRI ZA BIBLIA. Весь контент подкастов, включая эпизоды, графику и описания подкастов, загружается и предоставляется непосредственно компанией SIRI ZA BIBLIA или ее партнером по платформе подкастов. Если вы считаете, что кто-то использует вашу работу, защищенную авторским правом, без вашего разрешения, вы можете выполнить процедуру, описанную здесь https://ru.player.fm/legal.
Maarifa ya ki-Mungu na namna ya kuliishi kusudi lako
…
continue reading
119 эпизодов
Отметить все как (не)прослушанные ...
Manage series 3273506
Контент предоставлен SIRI ZA BIBLIA. Весь контент подкастов, включая эпизоды, графику и описания подкастов, загружается и предоставляется непосредственно компанией SIRI ZA BIBLIA или ее партнером по платформе подкастов. Если вы считаете, что кто-то использует вашу работу, защищенную авторским правом, без вашего разрешения, вы можете выполнить процедуру, описанную здесь https://ru.player.fm/legal.
Maarifa ya ki-Mungu na namna ya kuliishi kusudi lako
…
continue reading
119 эпизодов
Все серии
×Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. 2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. 3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. 4 Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. 5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki. 6 Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
1. Maombi ya kufunga yanaweza kukufanya uongezeke kiimani. Mathayo 17:21 ‘’ [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] ‘’ 2. Macho yako ya ndani yatakuwa yanaona vizuri. Zaburi 119:18 ‘’ Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako. ‘’ . 3. Mwili wako utakuwa umetiishwa. Wakolosai 3:5 ‘’ Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;‘’ 4. Kupokea maana ni ahadi ya MUNGU kujibu maombi yako. Yeremia 29:13 ‘’Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.'' Tena Biblia inasema ''Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;-Mathayo 7:7'' na kwa sababu MUNGU analiangalia neno lake alitimize basi hata aliposema tuombe ni hakika atajibu maana yeye hajipingi na Neno lake, labda tu sisi tuombe vibaya na tupungukiwe na imani katika maombi yetu. 5. Utamruhusu ROHO MTAKATIFU kukutumia. 1 Kor 12:11 ‘’ lakini kazi hizi zote huzitenda ROHO huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. ‘’ --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Maisha Mapya Katika Kristo 1 Kwa hiyo, ndugu zangu, nawasihi kwa rehema zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana. 2Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na ukamilifu. 3 Kwa ajili ya neema niliyopewa nawaambia kila mmoja miongoni mwenu, asijidhanie kuwa bora kuliko impasavyo, bali afikiri kwa busara kwa kulingana na kipimo cha imani Mungu aliyompa. 4Kama vile katika mwili mmoja tulivyo na viungo vingi, navyo viungo vyote havina kazi moja, 5vivyo hivyo na sisi tulio wengi, tu mwili mmoja katika Kristo, nasi kila mmoja ni kiungo cha mwenzake. 6Tuna karama zilizotofautiana kila mmoja kutokana na neema tuliyopewa. Kama ni unabii na tutoe unabii kwa kadiri ya imani. 7Kama ni kuhudumu na tuhudumu, mwenye kufundisha na afundishe, 8kama ni kutia moyo na atie moyo, kama ni kuchangia kwa ajili ya mahitaji ya wengine na atoe kwa ukarimu, kama ni uongozi na aongoze kwa bidii, kama ni kuhurumia wengine na afanye hivyo kwa furaha. Alama Za Mkristo Wa Kweli 9 Upendo lazima usiwe na unafiki. Chukieni lililo ovu, shikamaneni na lililo jema. 10Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa ndugu. Waheshimuni na kuwatanguliza wengine. 11Msiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana. 12Kuweni na furaha katika tumaini, katika dhiki kuweni na saburi, dumuni katika maombi. 13Changieni katika mahitaji ya watakatifu, wakaribisheni wageni. 14Wabarikini wale wanaowatesa, barikini wala msilaani. 15Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wale waliao. 16Kaeni kwa amani ninyi kwa ninyi. Msijivune, bali mwe tayari kushirikiana na wanyonge. Wala msiwe watu wenye kujivuna kwamba mnajua kila kitu. 17 Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote. 18Kama ikiwezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote. 19Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza,” asema Bwana. 20Badala yake: “Kama adui yako ana njaa, mlishe; kama ana kiu, mpe kinywaji. Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.” 21Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
1 Kor 16:9 kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Mistari mbalimbali ambayo Mungu amezungumza nasi katika maandiko kwenye Biblia,kuhusu kutokuogopa "USIOGOPE" --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
JIFUNZE MAARIFA MBALIMBALI YA KIMUNGU KUPITIA PLATFORM ZA SIRI ZA BIBLIA. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
YESU KARIBU ANARUDI --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
KUJIWEKA WAKFU UPYA MBELE ZA MUNGU NA MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE WA MANA MINISTRY --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Maana halisi ya kuokoka --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
SAA YA WOKOVU NI SASA --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
MUNGU ASIPOKUJIBU MAOMBI YAKO MUULIZE KWANINI: MWAKASEGE --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
maroho yaliyo ndani ya wote wanaotazama picha chafu za ngono/ukombozi upo bado --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
MAOMBI YA KUVUNJA MAAGANO NA MIKATABA YA KUZIMU --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
FAIDA 13 ZA MAOMBI YA USIKU --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Maarifa ya kiMungu --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Jifunze neno la Mungu katika maisha yako --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
MAMBO MUHIMU YANAYOUNDA MADHABAHU Mungu wa madhabahu Kuhani wa madhabahu Washirika wa madhabahu Kafara ya madhabahu Nguvu ya madhabahu --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. 29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. 30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; 31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. #sirizabiblia Youtube/siri za biblia --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Ndoto kwa kawaida ya wanaadamu katika ulimwengu wa mwili ni mambo unaunayoyaona wakati umelala mara nyingi ndoto utaota wakati umelala Aina za ndoto kwa tafsiri za ulimwengu wa kimwili - Ndoto unaota kwa sababu umechoka sana mara nyingi ukiota hivyo watu na wewe mwenyewe unasema kua ni ndoto tu kwa sababu ni uchovu - Ndoto unaota kwa sababu una mawazo kwa kitu kinakufanya ukifikirie sana mfano ajira au mke au mume ukiota mara nyingi unasema ni ndoto tu kwa sababu namuwaza sana au unawaza sana - Ndoto unaota kwa sababu umehadithiwa au kuambiwa kitu Fulani kabla haujalala harafu unaota hivyo hivyo. Sasa hayo yote ni katika Ulimwengu wa kimwili tuangalie katika ulimwengu war oho ndoto ni nini? - Ndoto maana yake ni ( Hesabu 12:6) BWANA akasema, “Sikilizeni maneno yangu: “Akiwapo nabii wa BWANA miongoni mwenu, ninajifunua kwake kwa maono, ninanena naye katika ndoto. Maana yake kwamba Mungu anaongea na watu wake kwa kupitia ndoto na maono ila watu wengi ukiota unasema ni ndoto tu Kila ndoto unayoota inawezekana ikawa inakuhusu wewe au ndugu,jirani,mwenza,rafiki au mtu yeyote ambaye Mungu anakuonesha kitu juu yake na ukiwa unafatilia ulichokiota kwa makini unatakiwa uishi katika ndoto au maono yako anayokunesha Mungu @siri za biblia www.sirizabiblia.com +255 758 708 804 --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Kuokoka ni jambo la lazima sana kwa kila anayehitaji uzima wa milele. Kuokoka kuanza na kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi kisha unaishi ukilitii Neno la MUNGU. Kwanini ni muhimu sana kuokoka? Biblia inasema baada ya kifo hukumu. Waebrania 9:27 ''Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;'' Anayetenda dhambi akifa na dhambi zake anaenda kuzimu. Mteule wa KRISTO mtakatifu akifa anaenda mbinguni. Wanadamu wengi wakionywa kwamba waache dhambi husema wanahukumiwa na hutoa sababu kwamba anayeweza kuwahukumu ni MUNGU tu. Hukumu ni Siku ya mwisho tu ila sasa ni maonyo tu na maonyo hayo yanaletwa na Neno la MUNGU kupitia watumishi, hivyo watumishi wakati mwingine huonekana kama wanahukumu kumbe wanawasaidia watu. Hakuna mwanadamu anayetakiwa kumhukumu mwanadamu mwenzeke. Nikisema acha uzinzi na usaliti wa ndoa maana ni dhambi sio nakuhukumu Bali nakuambia kweli ya MUNGU. Nikisema acha dhambi na okoka sasa ni kwa lengo la kukusaidia wewe. Ni mhimu sana kumpokea YESU na kuanza kuishi katika kusudi la MUNGU la wokovu. Baada ya kuokoka naomba utambue kwamba wewe umekuwa mtumishi wa MUNGU wa kuwasaidia na wengine ili waje kwenye wokovu. Biblia inasema kuhusu aliyeokoka kwamba; ''Kwa maana MMEOKOLEWA kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha MUNGU;-Waefeso 2:8'' Biblia inasema tuliompokea YESU kama Mwokozi tumeokolewa. Kuna watu hudai hakuna kuokoka duniani lakini Neno la MUNGU ndio kweli na kweli hiyo inasema kawmba tuliompokea YESU tumeokolewa na sio tutaokolewa bali tumeokolewa tayari. Kama hujaokolewa basi nakusihi okolewa leo kwa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na kuanza kuishi maisha matakatifu ya wokovu wa KRISTO ulio wa thamani sana. Baada ya kuokolewa naomba ujue mambo 7 muhimu haya yafuatayo. Hiki ndicho kiini cha somo langu la Leo kwamba ''Tumeokoka ili?'' @siri za biblia www.sirizabiblia.com +255 758 708 804 --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
S
SIRI ZA BIBLIA
Yesu akasema hivi katika Mathayo 6:12; mnaposali semeni hivi, ...utusamehe deni zetu kama nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.... Maandiko yanachomaanisha ni kwamba, ukiwa huna desturi ya kuwasamehe, hata wewe Mungu wa mbinguni hatakusamehe kabisa hata ukitubu kwa machozi ya damu. Kama yumkini unasamehe kwa kiasi, nawe dhambi zako husamehewa kiasi. Mat 6:14 Biblia inasema; "Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi". @sirizabiblia www.sirizabiblia.com +255 758 708 804 --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
S
SIRI ZA BIBLIA
1 MWAKASEGE:SHETANI ANAVYOTUMIA AKILI KUVURUGA MAISHA YA MTU 1:50:14
1:50:14
Прослушать Позже
Прослушать Позже
Списки
Нравится
Нравится
1:50:14MWAKASEGE:SHETANI ANAVYOTUMIA AKILI KUVURUGA MAISHA YA MTU --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
S
SIRI ZA BIBLIA
1 MWAKASEGE: FAIDA ZA KUPOKEA UPAKO WA MFALME WAKATI WA KUSHIRIKI MEZA YA BWANA 1:20:24
1:20:24
Прослушать Позже
Прослушать Позже
Списки
Нравится
Нравится
1:20:24MWAKASEGE: FAIDA ZA KUPOKEA UPAKO WA MFALME WAKATI WA KUSHIRIKI MEZA YA BWANA --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
MWAKASEGE: MISINGI YA UCHUMI WAKO INAHITAJI KUTENGENEZWA NA DAMU YA YESU website:www.sirizabiblia.com +255 758 708 804 whatssap only --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
FAIDA ZA IMANI UNAYOITUMIA KATIKA KUTOA SADAKA-MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE www.sirizabiblia.com +255 758 708 804 --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Baada ya vita ya 1948-1949 nchi jirani zilikataa kutambua dola la Israeli. Hali ya vita ikaendelea ingawa bila mapigano kati ya majeshi makubwa. Wanamgambo wa Wafedayin Wapalestina waliendelea kuvuka mpaka kutoka makambi ya wakimbizi na kushambulia vijiji vya Kiyahudi. Wanamgambo hao walipata mara nyingi silaha na mafunzo kutoka kwa majeshi ya Misri na Syria. Vita ya 1948-1949 ilisababisha ghasia na mashambulio dhidi ya Wayahudi walioishi katika nchi za Kiarabu. Nchi kadhaa za Kiarabu ziliweka sheria za ubaguzi dhidi ya Wayahudi. Hivyo katika miaka baada ya kuundwa kwa Israeli karibu Wayahudi wote waliondoka au walifukuzwa katika nchi za Kiarabu na kufika kama wakimbizi katika Israel, Marekani au Ulaya. Jumla ya wakimbizi hao Wayahudi karibu ililingana na idadi ya Waarabu waliofukuzwa kutoka Palestina. Hivyo idadi ya wananchi Wayahudi wa Israeli iliongezeka sana. Uhusiano mbaya kati ya Israeli na majirani Waarabu ulisababisha vita zaidi. Mwaka 1956 Israeli ilishambulia Misri katika vita ya Suez kufuatana na mpango wa pamoja na Ufaransa na Uingereza baada ya kuona ununuzi wa silaha nyingi na Misri. VITA VYA SIKU SITA. Madai ya Waisraeli yanaanzia katika misingi ya kidini ambapo katika Biblia (kitabu kitakatifu kwa Wakristo na Wayahudi), kitabu cha kwanza cha nabii Musa kiitwacho Mwanzo sura ya 12 inaonesha jinsi Ibrahim anavyoitwa na mwenyezi Mungu ili kumtumikia. Eneo hilo la Palestina (zamani lilijulikana kama Kaanani)ndiyo chimbuko la dini kuu tatu zenye msingi wa Ibrahim ambazo ni dini ya Wayahudi, Ukristo na baadaye Uislam. Dini ya wayahudi yenye misingi ya Biblia Agano la Kale likianza na vitabu vitano vya Musa (Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Mambo ya Walawi na Kumbukumbu la torati), Ukristo ukianza misingi kwenye Agano la Kale hadi Agano Jipya na Uislam ukishika vitabu vinne Tourat ya nabii Musa (a.s), Zabur ya nabii Dawood (a.s), Injili ya Issa bin Mariam (a.s.) au Yesu na Quran ya Muhamad (s.a.w) Ibrahim mwenyeji wa Uru wa Ulkadayo (Mesopotamia) leo Iraq wa kabila la Waebrania anahama kutoka Iraq na kwenda Haran Syria na baadaye kutelemkia Kaanani (Uyahudi) ambapo Mwenyezi Mungu anamtokea katika njozi na kumwapia Ibrahimu kuwa ardhi yote hiyo amepewa yeye na uzao wake na kuahidiwa baraka yaani kubarikiwa kwa kila atakaye mbariki na kwamba jamaa zote za dunia zitajibarikia. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Katika karne ya 19 idadi kubwa ya Wayahudi waliishi katika maeneo kadhaa ya Milki ya Urusi yaliyotwaliwa na milki hiyo mnamo 1800. Uadui dhidi ya Wayahudi ulitokea katika utawala wa Kirusi. Kuanzia mwaka 1880 kulitokea ghasia mbalimbali ambako Wayahudi walishambuliwa katika miji ya Urusi. Wimbi la pili la ghasia hizo zilizoitwa pogromu zilikatokea mwaka 1905, ambapo Wayahudi zaidi ya 2000 waliuawa mjini Odessa . Wakati ule Wayahudi wa Urusi walianza kuhamia nje: wengi wao walikwenda Marekani, lakini wachache walielekea Palestina. Mapogromu yalikuwa pia chanzo cha harakati mpya ya Uzayuni (Zionism) kati ya Wayahudi wa Ulaya. Uzayuni ulilenga kuwapa Wayahudi eneo maalum ili wapate kujenga upya taifa katika dola lao wenyewe, ambako wangekuwa wenyeji, si kundi la pekee katikati ya watu waliowadharau. Mwaka 1896 Theodor Herzl (1860-1904) aliandika kitabu "Dola la Wayahudi" alimodai kuundwa dola la pekee kwa ajili ya Wayahudi. Mkutano wa kwanza wa wafuasi wake ulichagua jina la "zion" ambalo lilikuwa jina asilia la mlima wa hekalu mjini Yerusalemu; wakachagua jina hilo kwa sababu linataja mahali patakatifu zaidi pa Uyahudi. Mkutano huo uliazimia kuwa "Uzayuni unalenga kuunda makazi salama yaliyokubaliwa rasmi kwa ajili ya taifa la Kiyahudi katika nchi ya Palestina". Wazayuni walikusanya pesa kote Ulaya wakanunua ardhi katika Palestina na kuanzisha vijiji kwa ajili ya Wayahudi waliohima huko. Palestina katika Milki ya Ottoman mwaka 1914 Vita ya Kwanza ya Dunia ilikwamisha mipango yote kwa sababu Palestina ilikuwa sehemu ya Milki ya Ottoman iliyoshiriki katika vita pamoja na Ujerumani na Austria dhidi ya Urusi, Ufaransa na Uingereza. Mwaka 1917 wakati ambapo jeshi la Uingereza lilifaulu kusogea mbele kutoka Misri na kuingia Palestina, waziri wa mambo ya nje Arthur James Balfour alitoa tamko la Balfour yaani tamko rasmi kuwa Uingereza inataka kusaidia mipango ya kuanzisha makazi ya Kiyahudi katika Palestina. Wakati uleule Waingereza waliwaahidi Waarabu kuundwa kwa dola la Kiarabu kwenye maeneo yaliyokaliwa nao katika Milki ya Ottoman. Lakini wakati huohuo walipatana na Ufaransa kuhusu ugawaji wa maeneo ya Kiarabu ya Milki ya Ottoman. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Inapatikana youtube,fuatilia https://youtu.be/4SslFrfEGCg --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
inapatikana youtube,fuatilia https://youtu.be/4SslFrfEGCg --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
inapatikana youtube https://youtu.be/4SslFrfEGCg --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Simulizi nzito zenye mikasa ya kufundisha na kukuza imani zetu kwa Mungu.Inapatikana youtube pia,andika siri za biblia ujifunze zaidi --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Amri Kumi Amri Kumi ni orodha ya amri kuu za Mungu katika Biblia . Za kwanza zinamhusu Mwenyezi Mungu mwenyewe, na zile zinazofuata mpaka mwisho zinahusu jirani, yaani binadamu wengine kuanzia wazazi . Toleo la awali linapatikana katika kitabu cha Kutoka 20:1-17. Toleo la pili liko katika Kumbukumbu la Torati 5:1-21. Amri hizi ni sehemu ya Torati ya Kiyahudi na kukubaliwa pia na Wakristo walio wengi kama amri zinazowahusu wao pia, tena kimsingi zinawadai watu wote. Hata hivyo wafuasi wa Yesu Kristo wanazishika kadiri ya utimilifu wake ulioletwa naye kama Agano Jipya . Mifano ya ukamilisho huo ni mafundisho ya Yesu katika Injili ya Mathayo 5:17-48. Hizi ni siri za biblia,subscribe channel hii ujifunze maarifa zaidi ya kiMungu..naitwa innocent mashauri naaaaaa Maneno yanayojulikana kama “Amri Kumi” yanapatikana katika vitabu vya Biblia "Kutoka" na "Kumbukumbu la Torati". --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Mathayo 25 1 Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. 2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. 3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; 4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. 5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. 6 Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. 7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. 8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. 9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. 10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. 11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. 12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi. 13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa. 14 Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. 15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. 16 Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano. 17 Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida. 18 Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. 19 Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao. 20 Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida. 21 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. 22 Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida. 23 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. 24 Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya; 25 basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako. 26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; 27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. 28 Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. 29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa. 30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. 31 Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; 32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijua… Siri za bibilia leo tuna muongozo ambao utakusaidia au itasaidia familia yako. Biblia inapozungumza habari ya watu waliofungwa wapate kufunguliwa, hii ina maana ya kuwa kuna watu wamefungwa chini ya utawala wa nguvu za giza katika ulimwengu wa Roho. Watu hawa wamefungwa kwenye magereza na Ibilisi. Tutambue ya kuwa Yesu aliposema amekuja kutuokoa hii inamaanisha kwamba kuna mahali ambako tusingeweza kujikwamua wenyewe bila nguvu yake yeye mwenywe kuingia kati yetu. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Mathayo 24 1 Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya hekalu. 2 Naye akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. 3 Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? 4 Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. 5 Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. 6 Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. 7 Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali. 8 Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu. 9 Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. 10 Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana. 11 Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. 12 Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. 13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. 14 Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. 15 Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu), 16 ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; 17 naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake; 18 wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake. 19 Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo! 20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. 21 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. 22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo. 23 Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. 24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. 25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. 26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. 27 Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 28 Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai. 29 Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Mathayo 23 1 Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema, 2 Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; 3 basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi. 4 Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao. 5 Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao; 6 hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, 7 na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi. 8 Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu. 9 Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. 10 Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo. 11 Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. 12 Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa. 13 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie. 14 [Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi.] 15 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe. 16 Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Mtu atakayeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amejifunga. 17 Wapumbavu ninyi na vipofu; maana ni ipi iliyo kubwa, ile dhahabu, au lile hekalu liitakasalo dhahabu? 18 Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga. 19 Vipofu ninyi; maana ni ipi iliyo kubwa, ile sadaka, au ile madhabahu iitakasayo sadaka? 20 Basi yeye aapaye kwa madhabahu, huapa kwa hiyo, na kwa vitu vyote vilivyo juu yake. 21 Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo, na kwa yeye akaaye ndani yake. 22 Naye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa yeye aketiye juu yake. 23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
MAMBO MUHIMU YANAYOUNDA MADHABAHU Ili uweze kushughulikia tatizo sugu lililoshikiliwa kwenye madhabahu ni lazima ufahamu vizuri kuwa madhabahu sio jina pekee bali ni muunganiko wa mambo sita (6) ambayo hayo yanafanya madhabahu kuwepo na kuwa na nguvu, mambo hayo ni kama yafuatayo:- Madhabahu yenyewe Kuhani wa madhabahu Kafara ya madhabahu Washirika wa madhabahu Mungu wa madhabahu Nguvu ya madhabahu Madhabahu yenyewe Madhabahu hujengwa na watu kwa kusudi la kufanya ibada kwa Mungu wanaye mwamini. Kwa kawaida kila mwanadamuanaamini kuwepo kwa nguvu ambayo ni kubwa kuliko nguvu ya kibinadamu (existence of super natural power). Ili kuwasiliana na nguvu hii mwanadamu inambidi kutengeneza utaratibu wa kuifikia nguvu hiyo (kujenga madhabahu). Iwe ni kwa upande wa nuru au giza madhabahu lazima ijengwe kwa jinsi ya mwili kabisa. Eliya alijenga madhabahu ya Bwana (1Wafalme 18: 32 “Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la Bwana; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu”) Vilevile makuhani wa shetani nao hujenga madhabahu 1Wafalme 16:33 “Ahabu akaifanya Ashera; Ahabu akazidi kumghadhibisha Bwana, Mungu wa Israeli, kuliko wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.” Ninachotaka ufahamu hapa ni kwamba madhabahu hujengwa kwa jinsi ya mwilini iwe ya Jehova au ya miungu. Kuhani wa madhabahu Kuhani wa madhabahu ni mtu anayejua taratibu za madhabahu na mwenye uwezo(nafasi au cheo kilichokubalika) wa kuleta vitu vya kiroho (Baraka au laana) kutoka ulimwengu wa roho kuingiza katika ulimwengu wa mwili na kutoa vitu (sadaka/kafara/manuizio) kutoka katika ulimwengu wa mwili kwenda katika ulimwengu wa roho a. Makuhani wa Jehova Katika uliwengu wa nuru kuhani ni mtu yoyote aliyempokea Yesu na kuzishika amri zake (Ufunuo 5:10“ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.” Vilevile kuhani anaweza kuwa mtu yoyote aliyejifunza taratibu za kiibada yak i-Mungu kama mchungaji, shemasi, mwinjilisti, askofu, paroko n.k. mfano katika Biblia tunamuona Melkizedeki alikuwa kuhani wa Jehova. Mwanzo 14:18 “Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.” b. Kuhani wa madhabahu za kishetani Katika ulimwengu wa giza kuhani ni mtu yoyote ambaye anamtumikia shetani kwa kujua au bila kujua kwa lengo la kuleta uharibifu, nasema kwa kujua au bila kujua kwani kuna watu wanaitumikia mizimu ya nyumbani kwao wakidhani wanafanya kawaida kama walivyofanya baba na babu zao (mfano kuchinja kila mwaka, kuomba kwenye makaburi), lakini bila wao kujua kuwa wameshakabidhiwa ukuhani wa madhabahu za kishetani. Watu hawa huja kushtuka pale mambo yanapowaendea vibaya kwa kukiuka kanuni za kimadhabahu bila wao kujua. Mfano wa makuhani wa madhabahu za kishetani katika biblia ni makuhani wa dagoni na baali. 1 Samweli 5:5 “Kwa hiyo makuhani wa Dagoni, na mtu awaye yote aingiaye nyumbani mwa Dagoni, hawakanyagi kizingiti cha nyumba ya Dagoni huko Ashdodi, hata leo.” 1Wafalme 18:25-26 “25 Eliya akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng’ombe mmoja, mkamtengeze kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini. 26 Wakamtwaa yule ng’ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya madhabahu waliyoifanya.” Kafara/sadaka ya madhabahu Madhabahu haiwezi kukamilika kama hakuna kafara kwasababu kila mungu/Mungu wa madhabahu huhitaji kafara. Haijalishi uko upande gani lazima unapoenda madhabahuni uende na kafara/sadaka. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Kumekuwa na mitazamo mingi ya tofauti tofauti ya namna ya kushughulikia matatizo sugu ambayo yamewakabili watoto wa Mungu kwa muda mrefu sana. Kuna watu wametaka kutoka katika umasikini kwa muda mrefu lakini hawajatoka mpaka sasa na hawajui tatizo limekaa wapi, wengine wametaka kutoka katika matatizo ya ndoa, wengine wametaka kuoa au kuolewa lakini mambo hayo yameshindikana kabisa hata kwa kufunga na kuomba hawajaweza kutoka katika matatizo hayo na mpaka sasa hawana majibu ya matatizo yao. Kuna watu familia zao zimekuwa na vifo vya kutatanisha au vya ghafla, wengine wamekuwa na magonjwa ya kutisha kutoka kizazi hadi kizazi na hata sasa hawana majibu ya maswali yao. Matatizo sugu huwa chanzo chake na hayatokei pasipo chanzo/sababu. Chanzo au msingi wa matatizo sugu ni kuvunjika kwa makubaliano (maagano/mikataba) yaliyoingiwa na pande mbili au zaidi, anayevunja makubaliano anaingia kwenye matatizo ambayo ni matokeo yaliyokubaliwa (kwa kujua au bila kujua) wakati wa kufunga mkataba/mikataba hiyo (Kumbukumbu 28:15-68 “15 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata…………..”). Kwa utaratibu na sheria za kiroho mikataba/maagano hayo hufanyika katika madhabahu ambazo ndio kiunganishi kati ya ulimwengu wa mwili na ulimwengu madhabahu hizi huonekana kwa macho ya kibinadamu (kwakuwa hujengwa katika ardhi) --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Kumekuwa na mitazamo mingi ya tofauti tofauti ya namna ya kushughulikia matatizo sugu ambayo yamewakabili watoto wa Mungu kwa muda mrefu sana. Kuna watu wametaka kutoka katika umasikini kwa muda mrefu lakini hawajatoka mpaka sasa na hawajui tatizo limekaa wapi, wengine wametaka kutoka katika matatizo ya ndoa, wengine wametaka kuoa au kuolewa lakini mambo hayo yameshindikana kabisa hata kwa kufunga na kuomba hawajaweza kutoka katika matatizo hayo na mpaka sasa hawana majibu ya matatizo yao. Kuna watu familia zao zimekuwa na vifo vya kutatanisha au vya ghafla, wengine wamekuwa na magonjwa ya kutisha kutoka kizazi hadi kizazi na hata sasa hawana majibu ya maswali yao. Matatizo sugu huwa chanzo chake na hayatokei pasipo chanzo/sababu. Chanzo au msingi wa matatizo sugu ni kuvunjika kwa makubaliano (maagano/mikataba) yaliyoingiwa na pande mbili au zaidi, anayevunja makubaliano anaingia kwenye matatizo ambayo ni matokeo yaliyokubaliwa (kwa kujua au bila kujua) wakati wa kufunga mkataba/mikataba hiyo (Kumbukumbu 28:15-68 “15 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata…………..”). Kwa utaratibu na sheria za kiroho mikataba/maagano hayo hufanyika katika madhabahu ambazo ndio kiunganishi kati ya ulimwengu wa mwili na ulimwengu madhabahu hizi huonekana kwa macho ya kibinadamu (kwakuwa hujengwa katika ardhi) --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Kumekuwa na mitazamo mingi ya tofauti tofauti ya namna ya kushughulikia matatizo sugu ambayo yamewakabili watoto wa Mungu kwa muda mrefu sana. Kuna watu wametaka kutoka katika umasikini kwa muda mrefu lakini hawajatoka mpaka sasa na hawajui tatizo limekaa wapi, wengine wametaka kutoka katika matatizo ya ndoa, wengine wametaka kuoa au kuolewa lakini mambo hayo yameshindikana kabisa hata kwa kufunga na kuomba hawajaweza kutoka katika matatizo hayo na mpaka sasa hawana majibu ya matatizo yao. Kuna watu familia zao zimekuwa na vifo vya kutatanisha au vya ghafla, wengine wamekuwa na magonjwa ya kutisha kutoka kizazi hadi kizazi na hata sasa hawana majibu ya maswali yao. Matatizo sugu huwa chanzo chake na hayatokei pasipo chanzo/sababu. Chanzo au msingi wa matatizo sugu ni kuvunjika kwa makubaliano (maagano/mikataba) yaliyoingiwa na pande mbili au zaidi, anayevunja makubaliano anaingia kwenye matatizo ambayo ni matokeo yaliyokubaliwa (kwa kujua au bila kujua) wakati wa kufunga mkataba/mikataba hiyo (Kumbukumbu 28:15-68 “15 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata…………..”). Kwa utaratibu na sheria za kiroho mikataba/maagano hayo hufanyika katika madhabahu ambazo ndio kiunganishi kati ya ulimwengu wa mwili na ulimwengu madhabahu hizi huonekana kwa macho ya kibinadamu (kwakuwa hujengwa katika ardhi) --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Mwa 6:5-9:17 inatufundisha kwamba Mungu anachukizwa na dhambi , hivyo anataka kuondoa maovu duniani ili nchi impendeze kama alivyokusudia alipoiumba. Kwa ajili hiyo zamani za Nuhu alileta maji yafunike dunia na kuzamisha waovu. Lakini alisalimisha waadilifu katika safina kubwa ya kutosha, halafu akafunga nao agano thabiti ( Eb 11:7). Kadiri ya Mtume Petro maji yanayokusudiwa kutakasa dunia yote ni yale ya ubatizo ( 1Pet 3:17-22), na safina ambayo iokoe watu ni Kanisa , ambalo kadiri ya Agano Jipya ni la lazima kwa wokovu kama vile ubatizo unaotuingiza ndani yake. Uso wa nchi ulipokwishatakaswa na maji njiwa akarukaruka akachuma tawi la mzeituni unaozaa matunda ya kutengenezea mafuta. Njiwa akaonekana tena juu ya maji siku ya ubatizo wa Yesu ambapo alipakwa Roho Mtakatifu na kuyatia maji nguvu ya kutakasa watu ( Mk 1:9-11; Tito 3:3-7). Maji na mafuta ndiyo mwanzo mpya kwa binadamu . Mara alipotoka safinani Nuhu alimtolea Mungu sadaka iliyompendeza hata akaahidi hataangamiza tena binadamu kila anapostahili. Sadaka hiyo ni mfano wa ile ya Yesu msalabani, inayoadhimishwa katika ekaristi , ikituondolea adhabu nyingi na kutuletea huruma ya Mungu, yaani nafasi na neema ya kutubu (Tito 2:11-14). Hatimaye kutakuwa na hukumu itakayobagua waadilifu na waovu kama siku za Nuhu ( Math 24:37-41). --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
SOMO: MAJITU (WANEFILI). ASILI YA MAJITU - WANEFILI NI KUTOKA WAPI ? NI WAJUMBE WA SHETANI WANAOJIINGIZA KATIKA KUSANYIKO AU USHIRIKA WA WANA WA MUNGU! 1. MAANA YA MAJITU. a. NI MAGUGU YALIYOPANDWA NA IBILISI KATIKA SHAMBA LA MUNGU (ULIMWENGUNI)? Mathayo 13: 24 Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda MBEGU NJEMA katika konde lake; 25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda MAGUGU KATIKATI YA NGANO, akaenda zake. 26 Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. 27 Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, BWANA, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? 28 Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye? 29 Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing'oa ngano pamoja nayo. 30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu. b. MAJITU HAYO YAPO KATIKA AINA KUU TATU. i. WAREFAI-majitu yenye urefu wa kati ya futi 8 hadi futi 12. Goliati alikuwa ni mfilisti mrefai mwenye urefu wa karibu futi 10 na uzito wa paundi 500. Maana ya Warefai ni “waliozaliwa kinyume na kawaida ya asili, wasio wa kawaida”. Kwa maana nyingine ni majitu(giant) au wafu(dead), roho, au mizimu(shade); na wala tafsiri yake siyo “kuanguka, kuharibu; wale wawaangukiao walio dhaifu, wale walioanguka kutoka mbinguni”. ii. WAANAKI-majitu yenye urefu wa kati ya futi 12 hadi futi 18. Mfalme Ogu wa bashani ni mfano wake. Yaliishi katika miji mikubwa yakiwa na wafalme na watawala. Yalionekana muda mfupi tu baada ya ghalika, na yalimiliki eneo la Shinari(Iraki), chini ya mtawala wao Nimrodi, yalijaribu kuhamasisha watu kujenga mnara ili kufika kwa Mungu(mnara wa Babeli). --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
SOMO: MAJITU (WANEFILI). ASILI YA MAJITU - WANEFILI NI KUTOKA WAPI ? NI WAJUMBE WA SHETANI WANAOJIINGIZA KATIKA KUSANYIKO AU USHIRIKA WA WANA WA MUNGU! 1. MAANA YA MAJITU. a. NI MAGUGU YALIYOPANDWA NA IBILISI KATIKA SHAMBA LA MUNGU (ULIMWENGUNI)? Mathayo 13: 24 Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda MBEGU NJEMA katika konde lake; 25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda MAGUGU KATIKATI YA NGANO, akaenda zake. 26 Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. 27 Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, BWANA, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? 28 Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye? 29 Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing'oa ngano pamoja nayo. 30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu. b. MAJITU HAYO YAPO KATIKA AINA KUU TATU. i. WAREFAI-majitu yenye urefu wa kati ya futi 8 hadi futi 12. Goliati alikuwa ni mfilisti mrefai mwenye urefu wa karibu futi 10 na uzito wa paundi 500. Maana ya Warefai ni “waliozaliwa kinyume na kawaida ya asili, wasio wa kawaida”. Kwa maana nyingine ni majitu(giant) au wafu(dead), roho, au mizimu(shade); na wala tafsiri yake siyo “kuanguka, kuharibu; wale wawaangukiao walio dhaifu, wale walioanguka kutoka mbinguni”. ii. WAANAKI-majitu yenye urefu wa kati ya futi 12 hadi futi 18. Mfalme Ogu wa bashani ni mfano wake. Yaliishi katika miji mikubwa yakiwa na wafalme na watawala. Yalionekana muda mfupi tu baada ya ghalika, na yalimiliki eneo la Shinari(Iraki), chini ya mtawala wao Nimrodi, yalijaribu kuhamasisha watu kujenga mnara ili kufika kwa Mungu(mnara wa Babeli). --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
S
SIRI ZA BIBLIA
1 CHRISTOPHER MWAKASEGE: WITO WA KUOMBEA MBEGU ZA MABADILIKO YA MSIMU MPYA KATIKA MIFUMO YA ULIMWENGU PART 2 43:04
CHRISTOPHER MWAKASEGE: WITO WA KUOMBEA MBEGU ZA MABADILIKO YA MSIMU MPYA KATIKA MIFUMO YA ULIMWENGU --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
S
SIRI ZA BIBLIA
1 CHRISTOPHER MWAKASEGE: WITO WA KUOMBEA MBEGU ZA MABADILIKO YA MSIMU MPYA KATIKA MIFUMO YA ULIMWENGU PART 1 41:54
CHRISTOPHER MWAKASEGE: WITO WA KUOMBEA MBEGU ZA MABADILIKO YA MSIMU MPYA KATIKA MIFUMO YA ULIMWENGU --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Mafundisho ya neno la Mungu kutoka kwa Mtumishi wake Mwalimu Christopher Mwakasege wa MANA MINISTRY --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Kaini kadiri ya Biblia ni jina la binadamu wa kwanza kuzaliwa na kuua. Kadiri ya kitabu cha Mwanzo (Biblia) katika Agano la Kale wana wawili wa kwanza wa Adamu na Hawa , majina yao Kaini na Habili , walitunza imani yao kwa Mungu wakamtolea sadaka . Habili aliitoa katika wanyama bora wa kundi lake, akiwa na hali ya unyenyekevu na imani, naye Mungu akampokea. Tabia ya Kaini ilikuwa ya kiburi , bila ya kumcha Mungu, kwa hiyo Mungu alimkataa (4:1-5; taz. Ebr 11:4; 1 Yoh 3:12). Tabia na maisha ya watoaji wa sadaka ina maana kuliko vitu wanavyovitoa, kwa hiyo Mungu alimwambia Kaini kuwa, akitaka Mungu ampokee, angepaswa kushinda dhambi iliyokuwa ikitaka kumwangamiza. Dhambi hiyo ilikuwa kama mnyama wa mwitu ajikunjaye na kuotea mlangoni, ili aweze kumshambulia mtu akitoka nje (4:6-7). Kaini hakushinda dhambi yake, na katika hasira ya wivu alimwua Habili. Tendo lake la kutwaa uzima wa ndugu yake lilidai kisasi kwa Mungu aliyetoa uhai ule. Kwa hiyo Mungu alimfukuza Kaini aende mbali na mahali walipoishi watu wengine. Ingawa Kaini alidumu katika hali ya kutotubu, Mungu katika huruma yake kubwa alimlinda asiuawe kwa kisasi (4:8-16). --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Lilith ni jina la mwanamke ambaye katika hadithi fulani za Mesopotamia ya kale anatajwa kama mungu mke ambaye anahusika na dhoruba akazaa majini . Biblia inasimulia jinsi dunia ilivyoumbwa na mwanzo wa binadamu . Katika maandiko hayo, masimulizi ya uumbaji yana changamoto kuyafahamu sawasawa, hususani kitabu cha Mwanzo 1:26 na Mwanzo 2. Uumbaji wa mwanamke unatajwa sehemu hizo mbili, lakini kwa namna tofauti, kwa kuwa ni visasili tofauti. Katika Mwa 1:26 Mungu aliwaumba Adamu na Eva sawia kwa sura na mfano wake. Katika Mwa 2 Mungu anamuumba Hawa baada ya kuchukua ubavu wa Adamu na kumfanya mwanamke. Katika Biblia Isa 34:14 tu inamtaja Lilith, na jina hilo linatafsiriwa pengine " Bundi ", sambamba na wanyama wengine saba wanaotajwa katika mstari huohuo na ule unaofuata. Hata hivyo kuanzia karne ya 10 BK wametokea watu wanaodai Lilith, si Hawa, ndiye mwanamke wa kwanza ulimwenguni naye aliumbwa na Mungu wakati mmoja na Adamu . Wanasema Lilith alifukuzwa na kukataliwa na Mungu baada ya kupatikana kuwa mwenye nguvu zaidi na mwenye akili zaidi ya Adamu na hakutii amri za Adamu . --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Mwanzo 1:1-25 BHN Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na dunia. Dunia ilikuwa bila umbo na tupu. Giza lilikuwa limefunika vilindi vya maji na roho ya Mungu ilikuwa ikitanda juu ya maji. Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa. Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza, mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza. Mungu akasema, “Anga liwe katikati ya maji, liyatenge maji sehemu mbili.” Mungu akalifanya anga, akayatenga maji yaliyo juu ya anga na yale yaliyo chini ya anga hilo. Ikawa hivyo. Mungu akaliita anga “Mbingu.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya pili. Mungu akasema, “Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, nchi kavu itokee.” Ikawa hivyo. Mungu akapaita mahali pakavu “Nchi” na kusanyiko la maji akaliita “Bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema. Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo. Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tatu. Mungu akasema, “Mianga na iweko angani, itenge mchana na usiku, ioneshe nyakati, majira, siku na miaka, na ingae angani na kuiangazia dunia.” Ikawa hivyo. Basi, Mungu akafanya mianga miwili mikubwa; ule mkubwa utawale mchana na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. Mungu akaiweka mianga hiyo angani iiangazie dunia, ipate kutawala mchana na usiku, na kuutenga mwanga na giza. Mungu akaona kuwa ni vyema. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya nne. Mungu akasema, “Maji na yatoe makundi ya viumbe hai na ndege waruke angani.” Basi, Mungu akaumba wanyama wakubwa sana wa baharini na aina zote za viumbe vyote hai viendavyo na kujaa majini; akaumba na aina zote za ndege wote. Mungu akaona kuwa ni vyema. Mungu akavibariki, akasema, “Zaeni, muongezeke, muyajaze maji ya bahari; nao ndege waongezeke katika nchi.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tano. Mungu akasema, “Nchi na itoe aina zote za viumbe hai, wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo na wanyama wa porini wa kila aina.” Ikawa hivyo. Basi, Mungu akafanya aina zote za wanyama wa porini, wanyama wa kufugwa, na viumbe vitambaavyo. Mungu akaona kuwa ni vyema. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
MWANZO 11 Mnara wa Babeli 1Kwanza, watu wote duniani walikuwa na lugha moja na walitumia maneno yaleyale. 2Basi, ikawa watu waliposafirisafiri kutoka mashariki, walifika katika nchi tambarare huko Shinari, wakakaa. 3Kisha wakaambiana, “Haya! Na tufyatue matofali, tuyachome moto vizuri.” Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. 4Wakasema, “Na tujijengee mji na mnara ambao kilele chake kitafika mbinguni ili tujipatie jina, tusije tukatawanyika duniani kote.” 5Ndipo Mwenyezi-Mungu akashuka chini kuuona mji huo na mnara walioujenga binadamu. 6Mwenyezi-Mungu akasema, “Tazama, watu hawa ni taifa moja na wote wana lugha moja; huu ni mwanzo tu wa yale watakayoyafanya. Lolote wanalokusudia kulifanya watafanikiwa. 7Haya, na tushuke chini na kuivuruga lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.” 8Hivyo, Mwenyezi-Mungu akawatawanya mahali pote duniani, nao wakaacha kuujenga ule mji. 9Mji huo ukaitwa Babeli, kwa sababu huko ndiko Mwenyezi-Mungu alikoivuruga lugha ya dunia yote, na kutoka huko akawatawanya watu kila mahali duniani. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni. 31 Tena kwa habari ya kiyama ya watu, hamjalisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema, 32 Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. 33 Na makutano waliposikia, walishangaa kwa mafunzo yake. 34 Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja. 35 Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu; 36 Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 40 Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii. 41 Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo? 42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi. 43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema, 44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako? 45 Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe? 46 Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Hata walipokaribia Yerusalemu, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu alipotuma wanafunzi wawili akiwaambia, 2 Enendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na mwana-punda pamoja naye; wafungueni mniletee. 3 Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; na mara huyo atawapeleka. 4 Haya yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, 5 Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda. 6 Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru, 7 wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake. 8 Watu wengi katika ule mkutano wakatandaza nguo zao njiani; na wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandaza njiani. 9 Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni. 10 Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu? 11 Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya. 12 Yesu akaingia ndani ya hekalu, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa; 13 akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi. 14 Na vipofu na viwete wakamwendea mle hekaluni, akawaponya. 15 Lakini wakuu wa makuhani na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao hekaluni, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi! Walikasirika, 16 wakamwambia, Wasikia hawa wasemavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa? 17 Akawaacha, akatoka nje ya mji mpaka Bethania, akalala huko. 18 Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa. 19 Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara. 20 Wanafunzi walipoona, walistaajabu, wakisema, Jinsi gani mtini umenyauka mara? 21 Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka, ukatupwe baharini, litatendeka. 22 Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu. 2 Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu. 3 Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi; 4 na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda. 5 Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile. 6 Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi? 7 Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu. 8 Kulipokuchwa, yule bwana wa shamba akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira wao, ukianzia wa mwisho hata wa kwanza. 9 Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari. 10 Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari. 11 Basi wakiisha kuipokea, wakamnung'unikia mwenye nyumba, 12 wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa. 13 Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari? 14 Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe. 15 Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema? 16 Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho. 17 Hata Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalemu, aliwachukua wale wanafunzi kumi na wawili faraghani; na njiani akawaambia, 18 Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemu; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa wakuu wa makuhani na waandishi; nao watamhukumu afe; 19 kisha watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumsulibisha; na siku ya tatu atafufuka. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
MATHAYO 19 Kuhusu talaka 1Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, alitoka Galilaya, akaenda Yudea, ngambo ya mto Yordani. 2Watu wengi walimfuata huko, naye akawaponya. 3Mafarisayo kadhaa walimjia, wakamwuliza kwa kumtega, “Je, ni halali mume kumpa talaka mkewe kwa kisa chochote?” 4Yesu akawajibu, “Je, hamkusoma katika Maandiko Matakatifu kwamba Mungu aliyemuumba mtu tangu mwanzo alimfanya mwanamume na mwanamke, 5na akasema: ‘Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja?’ 6Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja. Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asikitenganishe.” 7Lakini wao wakamwuliza, “Kwa nini basi, Mose alituagiza mwanamke apewe hati ya talaka na kuachwa?” 8Yesu akawajibu, “Mose aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. 9Lakini haikuwa hivyo tangu mwanzo. Basi nawaambieni, yeyote atakayemwacha mke wake isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, akaoa mke mwingine, anazini.” 10Wanafunzi wake wakamwambia, “Ikiwa mambo ya mume na mkewe ni hivyo, ni afadhali kutooa kabisa.” 11Yesu akawaambia, “Si wote wanaoweza kulipokea fundisho hili, isipokuwa tu wale waliojaliwa na Mungu. 12Maana kuna sababu kadhaa za kutoweza kuoa: Wengine ni kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine kwa sababu wamefanywa hivyo na watu, na wengine wameamua kutooa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee.” Yesu anawabariki watoto wadogo (Marko 10:13-16; Luka 18:15-17) 13Kisha watu wakamletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono na kuwaombea. Lakini wanafunzi wakawakemea. 14Yesu akasema, “Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie; maana ufalme wa mbinguni ni wa watu walio kama watoto hawa.” 15Basi, akawawekea mikono, kisha akaondoka mahali hapo. Kijana tajiri (Marko 10:17-31; Luka 18:18-30) 16Mtu mmoja alimjia Yesu, akamwuliza, “Mwalimu, nifanye kitu gani chema ili niupate uhai wa milele?” 17Yesu akamwambia, “Mbona unaniuliza kuhusu jambo jema? Kuna mmoja tu aliye mwema. Ukitaka kuingia katika uhai, shika amri.” 18Yule mtu akamwuliza, “Amri zipi?” Yesu akasema, “Usiue, Usizini, Usiibe, Usitoe ushahidi wa uongo, 19Waheshimu baba yako na mama yako; na, Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.” 20Huyo kijana akamwambia, “Hayo yote nimeyazingatia; nifanye nini zaidi?” 21Yesu akamwambia, “Kama unapenda kuwa mkamilifu, nenda ukauze mali yako, uwape maskini fedha hiyo, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo unifuate.” 22Huyo kijana aliposikia hayo, akaenda zake akiwa mwenye huzuni, maana alikuwa na mali nyingi. 23Hapo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kweli nawaambieni itakuwa vigumu sana kwa tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. 24Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.” 25Wale wanafunzi waliposikia hivyo walishangaa sana, wakamwuliza, “Ni nani basi, awezaye kuokoka?” 26Yesu akawatazama, akasema, “Kwa binadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote huwezekana.” 27Kisha Petro akasema, “Na sisi je? Tumeacha yote tukakufuata; tutapata nini basi?” 28Yesu akawaambia, “Nawaambieni kweli, Mwana wa Mtu atakapoketi katika kiti chake cha enzi kitukufu katika ulimwengu mpya, nyinyi mlionifuata mtaketi katika viti kumi na viwili mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli. 29Na kila aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi, na kupata uhai wa milele. 30Lakini walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
21 Kisha Petro akamwendea Yesu, akamwuliza, “Je, ndugu yangu akinikosea, nimsamehe mara ngapi? Mara saba?” 22 Yesu akamjibu, “Sisemi mara saba tu, bali sabini mara saba. 23 Ndiyo maana Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyeamua kukagua hesabu za watumishi wake. 24 Ukaguzi ulipoanza, akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni la fedha talanta elfu kumi. 25 Mtu huyo hakuwa na chochote cha kulipa; hivyo bwana wake aliamuru wauzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vitu vyote alivyokuwa navyo, ili deni lilipwe. 26 Basi, huyo mtumishi akapiga magoti mbele yake, akasema, Unisubiri nami nitakulipa deni lote. 27 Yule bwana alimwonea huruma, akamsamehe lile deni, akamwacha aende zake. 28 “Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake fedha denari mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akisema, Lipa deni lako! 29 Huyo mtumishi mwenzake akapiga magoti, akamwomba, Unisubiri nami nitalipa deni langu lote. 30 Lakini yeye hakutaka, bali alimtia gerezani mpaka hapo atakapolipa lile deni. 31 “Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana, wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia. 32 Hapo yule bwana alimwita huyo mtumishi, akamwambia, Wewe ni mtumishi mbaya sana! Uliniomba, nami nikakusamehe deni lako lote. 33 Je, haikukupasa nawe kumhurumia mtumishi mwenzako kama nilivyokuhurumia? 34 “Basi, huyo bwana alikasirika sana, akamtoa huyo mtumishi aadhibiwe mpaka hapo atakapolipa deni lote. 35 Na baba yangu aliye mbinguni atawafanyieni vivyo hivyo kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kwa moyo wake wote.” --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Mazungumzo mazito ya mahusiano na ndoa katika studio zetu tukiwa na Dr love. hii ni sehemu ya kwanza{3},fuatilia kwa makini ujifunze zaidi. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Jifunze maarifa mbalimbali ya kiMungu kupitia siri za biblia, https://youtu.be/3hKE7v7b43M --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Bustani ya Gethsemane , mahali ambapo jina lake kwa kweli linamaanisha "vyombo vya mafuta," iko kwenye mteremko wa Mlima wa Mizeituni kando ya bonde la Kidron kutoka Yerusalemu. Bustani ya miti ya mizeituni ya kale imesimama pale hadi leo. Yesu mara nyingi alikwenda Gethsemane pamoja na wanafunzi Wake kuomba (Yohana 18: 2). Matukio maarufu sana huko Gethsemane yalitokea usiku kabla ya kusulubiwa kwake wakati Yesu alipotolewa. Kila mmoja wa waandishi wa Injili anaelezea matukio ya usiku huo yakiwa na tofauti kidogo, hivyo kusoma akaunti nne (Mathayo 26: 36-56, Marko 14: 32-52; Luka 22: 39-53; Yohana 18: 1-11) yatatoa picha sahihi ya usiku huo muhimu katika ukamilifu wake. Jioni ilipoingia, baada ya Yesu na wanafunzi wake kusherehekea pasaka, walikuja katika bustani. Wakati fulani, Yesu alichukua watatu kati yao-Petro, Yakobo na Yohana -kwenda mahali pa kutengwa na wengine. Hapa Yesu aliwaomba wakeshe pamoja naye na kuomba ili wasianguke katika majaribu (Mathayo 26:41), lakini walilala. Mara mbili, Yesu aliwafufua na kuwakumbusha kuomba ili wasiingie katika majaribu. Hili lilikuwa la kushangaza hasa kwa sababu Petro alianguka katika majaribu baadaye usiku huo wakati mara tatu alikana hata kumjua Yesu. Yesu alihamia njia kidogo kutoka kwa wanaume watatu kuomba, na mara mbili akamwomba Baba yake aondoe kikombe cha ghadhabu alichotaka kunywa, lakini kila wakati aliwasilisha mapenzi ya Baba. Alikuwa "na huzuni sana hadi kufa" (Mathayo 26:38), lakini Mungu alimtuma malaika kutoka mbinguni kumtia nguvu (Luka 22:43). Baada ya hayo, Yuda Iskarioti, msaliti, alifika pamoja na "umati" wa askari, makuhani wakuu, Mafarisayo, na watumishi kumshika Yesu. Yuda alimtambua kwa ishara ya awali ya busu ambayo alimpa Yesu. Alijaribu kulinda Yesu, Petro akachukua upanga na kumshambulia mtu mmoja aitwaye Malko, mtumishi wa kuhani mkuu, akakata sikio. Yesu alimkemea Petro na kumponya masikio ya mtu. Inashangaza kwamba kushuhudia muujiza huu wa ajabu wa uponyaji haukuwa na athari kwa umati. Wala hawakutetemeka kwa nguvu yake ya kushangaza ya nguvu kama inavyoelezwa katika Yohana 18: 5-6, ambapo ama kwa utukufu wa kuonekana kwake, au kwa nguvu ya maneno Yake, au wote wawili, waliwa kama watu wafu, wakianguka chini. Hata hivyo, walimkamata na kumchukua kwa Pontio Pilato, wakati wanafunzi walitawanyika kwa hofu kwa maisha yao. Matukio yaliyotokea katika Bustani ya Gethsemane yamebadilishwa kupitia karne nyingi. Tamaa ambayo Yesu alionyesha katika usiku huo muhimu umeonyeshwa katika muziki, vitabu, na filamu kwa karne nyingi. Kutoka karne ya 16, wakati Bach aliandika oratorios mbili nzuri kulingana na injili za Mathayo na Yohana, hadi siku ya sasa na filamu Passion ya Kristo, hadithi ya usiku huu wa ajabu umeambiwa tena na tena. Hata lugha yetu imeathiriwa na matukio haya, kutupa maneno kama "yeye anayeishi kwa upanga hufa kwa upanga" (Mathayo 26:52); "Roho ni tayari, lakini mwili ni dhaifu" (Marko 14:38); na "matone ya jasho ya damu" (Luka 22:44). Kwa kweli, athari muhimu zaidi ya usiku huu ilikuwa nia ya Mwokozi wetu kufa msalabani mahali petu ili kulipa adhabu ya dhambi zetu. Mungu,"Yeye Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye" (2 Wakorintho 5:21). Hii ni injili ya Yesu Kristo. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Mazungumzo mazito ya mahusiano na ndoa katika studio zetu tukiwa na Dr love. hii ni sehemu ya kwanza{2},fuatilia kwa makini ujifunze zaidi. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
YOHANA 18 Yesu Akamatwa (Mathayo 26:47-56; Marko 14:43-50; Luka 22:47-53) 1 Yesu alipomaliza kuomba, akaondoka na wanafunzi wake wakavuka Bonde la Kidroni. Upande wa pili palikuwa na bustani, yeye na wanafunzi wake wakaingia humo. 2 Basi Yuda, yule aliyemsaliti alipafahamu mahali hapo kwani Yesu alikuwa akikutana humo na wanafunzi wake mara kwa mara. 3Hivyo Yuda akaja bustanini. Aliongoza kikosi cha askari wa Kirumi, na baadhi ya maafisa kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo. Nao walikuwa wamechukua taa, mienge na silaha. 4 Yesu akijua yale yote yatakayompata, akajitokeza mbele yao akawauliza, “Mnamtafuta nani?” 5 Wao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.” Yesu akawajibu, “Mimi ndiye.” Yuda, yule aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao. 6Yesu alipowaambia, “Mimi ndiye,” walirudi nyuma na kuanguka chini! 7 Akawauliza tena, “Mnamtafuta nani?” Nao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.” 8Yesu akawaambia, “Nimekwisha kuwaambia kuwa, mimi ndiye; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa watu waende zao.” 9Hii ilikuwa ili litimie lile neno alilosema, “Sikumpoteza hata mmoja miongoni mwa wale ulionipa.” 10 Simoni Petro, aliyekuwa na upanga, akaufuta na kumkata sikio la kuume mtumishi wa kuhani mkuu. Jina la mtumishi huyo aliitwa Malko. 11 Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Je, hainipasi kukinywea kikombe alichonipa Baba?” YOHANA 18 Yesu Akamatwa (Mathayo 26:47-56; Marko 14:43-50; Luka 22:47-53) 1 Yesu alipomaliza kuomba, akaondoka na wanafunzi wake wakavuka Bonde la Kidroni. Upande wa pili palikuwa na bustani, yeye na wanafunzi wake wakaingia humo. 2 Basi Yuda, yule aliyemsaliti alipafahamu mahali hapo kwani Yesu alikuwa akikutana humo na wanafunzi wake mara kwa mara. 3Hivyo Yuda akaja bustanini. Aliongoza kikosi cha askari wa Kirumi, na baadhi ya maafisa kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo. Nao walikuwa wamechukua taa, mienge na silaha. 4 Yesu akijua yale yote yatakayompata, akajitokeza mbele yao akawauliza, “Mnamtafuta nani?” 5 Wao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.” Yesu akawajibu, “Mimi ndiye.” Yuda, yule aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao. 6Yesu alipowaambia, “Mimi ndiye,” walirudi nyuma na kuanguka chini! 7 Akawauliza tena, “Mnamtafuta nani?” Nao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.” 8Yesu akawaambia, “Nimekwisha kuwaambia kuwa, mimi ndiye; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa watu waende zao.” 9Hii ilikuwa ili litimie lile neno alilosema, “Sikumpoteza hata mmoja miongoni mwa wale ulionipa.” 10 Simoni Petro, aliyekuwa na upanga, akaufuta na kumkata sikio la kuume mtumishi wa kuhani mkuu. Jina la mtumishi huyo aliitwa Malko. 11 Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Je, hainipasi kukinywea kikombe alichonipa Baba?” --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
S
SIRI ZA BIBLIA
1 LOVE TALK: MAPIGO 6 BAADA YA ADAM KULA TUNDA,YANAMTESA MWANAUME MPAKA LEO {sehemu ya kwanza} 10:02
Mazungumzo mazito ya mahusiano na ndoa katika studio zetu tukiwa na Dr love. hii ni sehemu ya kwanza{1},fuatilia kwa makini ujifunze zaidi. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
1. Mathayo 18:19,20 “Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao” Nampenda Bwana Yesu. Yani kila tukutanikapo wanadamu wawili huwa si wawili tena bali tupo watatu. Maana Bwana Yesu hujihudhurisha kuja kuchukua maombi yetu ampe Baba. 2. Marko 11:22-24 “Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu” 3. Yoh. 14:13,14 ‘Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya’ Msisitizo: – Bwana Yesu anasema lolote tutakaloomba! 4. Yoh. 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. ” Kukaa ndani ya Kristo na maneno yake kukaa ndani yetu huo ni ushirika katika mahusiano yetu na Mungu. Ni ushirika wa kudumu. Ushirika wa kila siku. Ni ushirika ambao ulianzishwa pale msalabani na Kristo mwenyewe. Damu yake ilipomwagika pale msalabani kwa ajili ya kutusafisha dhambi zetu, ilianzisha mahusiano yasiyo na kikomo. Kumuamini Bwana Yesu na kumkiri kama Bwana na Mwokozi wa maisha yetu ni mwanzo wa mahusiano hayo ya kudumu katika Kristo. Kuokoka ni hatua ya mwanzo. Na tunapaswa kuendelea na mahusiano na Kristo kwa Roho Mtakatifu. 5. Yoh. 15:16 “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni” 6. Yoh 16:23,24 “Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. - Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. -” Hakuna masharti ya NINI TUOMBE ila kuna masharti ya NAMNA YA KUOMBA: i. Kupitia jina la Yesu ii. Mtu aombaye awe na mahusiano na Mungu iii. Mwombaji awe na Imani Ubarikiwe sana. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
CHRISTOPHER MWAKASEGE: UHUSIANO WA MAOMBI YA TOBA KWA MUNGU NA MABADILIKO {2} --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Mathayo 17 1 Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani; 2 akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru. 3 Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye. 4 Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. 5 Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye. 6 Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana. 7 Yesu akaja, akawagusa, akasema, Inukeni, wala msiogope. 8 Wakainua macho yao, wasione mtu ila Yesu peke yake. 9 Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu. 10 Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? 11 Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote, 12 ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao. 13 Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji. 14 Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti, akisema, 15 Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. 16 Nikamleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya. 17 Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. 18 Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile. 19 Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa? 20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. 21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] 22 Nao walipokuwa wakikaa Galilaya, Yesu akawaambia, Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua, na siku ya tatu atafufuka. 23 Wakasikitika sana. 24 Hata walipofika Kapernaumu, wale watozao nusu-shekeli walimwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi nusu-shekeli? Akasema, Hutoa. 25 Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni? 26 Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru. 27 Lakini tusije tukawakwaza, enenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Jifunze maarifa ya kiMungu kutoka kwa Mwalimu Mwakasege --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Mafundisho ya neno la Mungu kutoka kwa mtumishi wake Mwalimu Christopher Mwakasege wa MANA Ministry --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
1 Wathesalonike 4:13-18 BHN Ndugu, twataka mjue ukweli kuhusu wale ambao wamekwisha fariki dunia, ili msipatwe na huzuni kama watu wengine wasio na matumaini. Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini. Hili tunalowaambieni ni fundisho la Bwana, kwamba sisi tulio hai, ambao tutakuwa tumebaki wakati Bwana atakapokuja, hakika hatutawatangulia wale waliokwisha fariki dunia. Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai wakati huo tutakusanywa pamoja nao katika mawingu kumlaki Bwana hewani. Na hivyo tutakuwa daima pamoja na Bwana. Basi, farijianeni kwa maneno haya. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
S
SIRI ZA BIBLIA
1 MATHAYO 16: KUNA WATU HAWATAONJA MAUTI,HATA WATAKAPOMWONA MWANA WA ADAM AKIJA KATIKA UFALME WAKE 4:10
Mathayo 16 1 Wakamjia Mafarisayo na Masadukayo, wakamjaribu, wakamwomba awaonyeshe ishara itokayo mbinguni. 2 Akajibu, akawaambia, [Kukiwa jioni, mwasema, Kutakuwa na kianga; kwa maana mbingu ni nyekundu. 3 Na asubuhi, mwasema, Leo kutakuwa na dhoruba; kwa maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa mbingu; lakini, je! Ishara za zamani hizi hamwezi kuzitambua?] 4 Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha, akaenda zake. 5 Nao wanafunzi wakaenda hata ng'ambo, wakasahau kuchukua mikate. 6 Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo. 7 Wakabishana wao kwa wao, wakisema, Ni kwa sababu hatukuchukua mikate. 8 Naye Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani chache, kwa sababu hamna mikate? 9 Hamjafahamu bado, wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa wale elfu tano, na vikapu vingapi mlivyoviokota? 10 Wala ile mikate saba kwa watu elfu nne, na makanda mangapi mliyoyaokota? 11 Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si kwa sababu ya mkate naliwaambia? Ila jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo. 12 Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo. 13 Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? 14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. 15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? 16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. 17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. 19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. 20 Ndipo alipowakataza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu ye yote ya kwamba yeye ndiye Kristo. 21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. 22 Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. 23 Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu. 24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. 25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. 26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? 27 Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 28 Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Yesu aliuita ule umati wa watu, akawaambia, “Sikilizeni, mkaelewe! 11Kitu kinachomtia mtu unajisi si kile kiingiacho kinywani, bali kile kitokacho kinywani. Hicho ndicho kimtiacho mtu unajisi.” 12Kisha wanafunzi wakamwendea, wakamwambia, “Je, unajua kwamba Mafarisayo walichukizwa waliposikia maneno yako?” 13Lakini yeye akawajibu, “Kila mmea ambao Baba yangu aliye mbinguni hakupanda, utangolewa. 14Waacheni wenyewe! Wao ni vipofu, viongozi wa vipofu; na kipofu akimwongoza kipofu, wote wawili hutumbukia shimoni.” 15Petro akasema, “Tufafanulie huo mfano.” 16Yesu akasema, “Hata nyinyi hamwelewi? 17Je, hamwelewi kwamba kila kinachoingia kinywani huenda tumboni na baadaye hutolewa nje chooni? 18Lakini mambo yatokayo kinywani hutoka moyoni, na hayo ndiyo yanayomtia mtu unajisi. 19Maana moyoni hutoka mawazo ya uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na kashfa. 20Hayo ndiyo yanayomtia mtu unajisi. Lakini kula chakula bila kunawa mikono hakumtii mtu unajisi.” --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
WARUMI 6:8 Lakini ikiwa tumekufa na Kristo, tunaamini kwamba pia tutaishi pamoja naye. 9 Kama tujuavyo, Kristo alikwisha kufufu liwa kutoka kwa wafu kwa hiyo hafi tena; kifo hakina mamlaka juu yake tena. 10 Alikufa kwa ajili ya dhambi mara moja tu, lakini maisha anayoishi anamwishia Mungu. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
KUSUDI LA MUNGU ni hali ambayo Mungu ametuwekea wanadamu katika maisha yetu ili kuweza kutimia kwa jambo fulani ndani yetu.Kitabu cha Mwanzo 1:1...... kinaelezea jinsi uumbaji wa Mungu kwa vitu na binadamu kusudi la Mungu katika maisha yetu si kuishi ya maisha ya mateso aliituumba ili tutawale KUISHI NA KUTAWALA Akatuumba kwa mfano wake ili tuishi ndani yake kwa kusudi lake kuu.Ili uweze kufanikiwa katika maisha yako ishi ndani ya kusudi la Mungu afu utaona ushindi juu yako. Yeremia 1:4-5-8 Isaya41:10 ILI UWEZE KULIISHI KUSUDI LA MUNGU (VITU VYA KUZINGATIA) 1. KULIISHI NENO(NENO LA MUNGU) Yoh 1;1 Yoh 4;24 Yoh 6:63 2. UTII Mwanzo 12:1-3 Isaya 1:19-20 3.KUWA NA MOYO WA NYAMA(KUNYENYEKEA) EZEKIEL 36:26-27 Ø Moyo ulioshuka Ø Moyo wa utii Ø Moyo mpya uliobeba vitu vipya Ø Moyo wenye hofu ya Mungu Ø Moyo usiojihesabia haki Isaya 57:15 Ø Moyo uliotayari kuendeshwa na roho na Mungu. 4.KUWA NA IMANI Ebrania 11:1 --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Mafundisho ya neno la Mungu kutoka kwa mtumishi wa Mungu Mwinjilisti Andulile katika kanisa la Mito ya Baraka.kipindi cha kuomboleza kitaifa kwa kuondokewa na Rais wetu mpendwa John Magufuli --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
KUSUDI LA MUNGU ni hali ambayo Mungu ametuwekea wanadamu katika maisha yetu ili kuweza kutimia kwa jambo fulani ndani yetu.Kitabu cha Mwanzo 1:1...... kinaelezea jinsi uumbaji wa Mungu kwa vitu na binadamu kusudi la Mungu katika maisha yetu si kuishi ya maisha ya mateso aliituumba ili tutawale KUISHI NA KUTAWALA Akatuumba kwa mfano wake ili tuishi ndani yake kwa kusudi lake kuu.Ili uweze kufanikiwa katika maisha yako ishi ndani ya kusudi la Mungu afu utaona ushindi juu yako. Yeremia 1:4-5-8 Isaya41:10 ILI UWEZE KULIISHI KUSUDI LA MUNGU (VITU VYA KUZINGATIA) 1. KULIISHI NENO(NENO LA MUNGU) Yoh 1;1 Yoh 4;24 Yoh 6:63 2. UTII Mwanzo 12:1-3 Isaya 1:19-20 3.KUWA NA MOYO WA NYAMA(KUNYENYEKEA) EZEKIEL 36:26-27 Ø Moyo ulioshuka Ø Moyo wa utii Ø Moyo mpya uliobeba vitu vipya Ø Moyo wenye hofu ya Mungu Ø Moyo usiojihesabia haki Isaya 57:15 Ø Moyo uliotayari kuendeshwa na roho na Mungu. 4.KUWA NA IMANI Ebrania 11:1 --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Mafundisho ya neno la Mungu kutoka kwa mtumishi wa Mungu Mwinjilisti Andulile,katika kipindi cha maombolezo ya kitaifa kwa taifa la Tanzania. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Somo la sadaka kutoka kwa mtumishi wa Mungu Mwalimu Mwakasege --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
3 Kabla ya wakati huu, Herode alimkamata Yohana. Akamfunga kwa minyororo na kumweka gerezani. Alimkamata Yohana kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, kaka yake Herode. 4 Yohana alikuwa amemwambia, “Si sahihi kwako kumwoa Herodia.” 5 Herode alitaka kumwua, lakini aliwaogopa watu. Waliamini kuwa Yohana alikuwa nabii. 6 Siku ya kuzaliwa Herode, bintiye Herodia[ a ] alicheza mbele yake na kundi lake. Herode alifurahishwa naye sana. 7 Hivyo aliapa kuwa atampa kitu chochote atakachotaka. 8 Herodia alimshawishi binti yake kitu cha kuomba. Hivyo bintiye akamwambia Herode, “Nipe hapa kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sahani kubwa.” 9 Mfalme Herode alihuzunika sana. Lakini alikuwa ameahidi kumpa binti kitu chochote alichotaka. Na watu waliokuwa wakila pamoja na Herode walikuwa wamesikia ahadi yake. Hivyo Herode aliamuru kitu ambacho alikuwa ameomba apatiwe. 10 Akawatuma wanaume gerezani, ambako walikikata kichwa cha Yohana. 11 Na watu wakakileta kichwa cha Yohana kwenye sahani kubwa na kumpa yule msichana. Kisha yeye akakipeleka kichwa kwa mama yake, Herodia. 12 Wafuasi wa Yohana wakaja na kuuchukua mwili wa Yohana na kuuzika. Kisha wakaenda na kumwambia Yesu kilichotokea. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande mbili tofauti. Kama tuna upendo kwa MUNGU inatupasa sana kushirikiana na MUNGU na kuwasiliana na MUNGU Mara kwa Mara. Mawasiliano hayo ni maombi . Lakini maombi tu hayawezi kuzaa matunda kama sio maombi ya imani. Kama kuna mambo matano(5) muhimu katika maombi yako basi ni hivi: =Jina la YESU KRISTO(Yohana 14:14), =Damu ya YESU KRISTO(Ufunuo 12:11), = Neno la MUNGU la ufunuo wa ROHO MTAKATIFU(Zaburi 107:20), =Nguvu za ROHO MTAKATIFU(Luka 1:35a) =Na Kuomba kwa imani(Waebrania 11:6) --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Somo la sadaka kutoka kwa mtumishi wa Mungu Mwakasege --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Wafuasi wake wakamwendea Yesu na kumuuliza, “Kwa nini unatumia simulizi hizi kuwafundisha watu?” 11 Yesu akawajibu, “Mungu amewapa ninyi ujuzi wa kuelewa siri za ufalme wa Mungu, lakini hajawapa watu hawa wengine ujuzi huu. 12 Kisha akawaambia, ‘Zingatieni kwa makini kile mnachokisikia. Kwani jinsi mnavyosikiliza kwa makini, ndivyo mtakavyoelewa na kuzidi kuelewa. Kwa kuwa kila aliye na uelewa kidogo ataongezewa zaidi. Lakini wale wasiosikiliza kwa makini watapoteza hata ule uelewa mdogo walio nao.’ 13 Ndiyo sababu ninatumia simulizi hizi kuwafundisha watu: Wanaona, lakini hakika hawaoni. Wanasikia, lakini hakika hawasikii au kuelewa. 14 Hiyo inathibitisha alichosema nabii Isaya kuhusu wao kuwa kweli: ‘Ninyi watu mtasikia na kusikia, lakini hamtaelewa. Mtatazama na kutazama, lakini hakika hamtaona. 15 Ndiyo, akili za watu hawa sasa zimefungwa. Wana masikio, lakini hawasikii vizuri. Wana macho, lakini wameyafumba. Iwapo akili zao zisingekuwa zimefungwa, wangeona kwa macho yao; wangesikia kwa masikio yao; Iwapo wangeelewa kwa akili zao. Kisha wangenigeukia na kuponywa.’ 16 Bahati gani mliyonayo ninyi. Mnaelewa mnachokiona kwa macho yenu. Na mnaelewa mnachosikia kwa masikio yenu. 17 Ninaweza kuwathibitishia, manabii na watakatifu wengi walitaka kuona mnayoyaona. Lakini hawakuyaona. Walitaka kusikia mnayosikia sasa. Lakini hawakuyasikia. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande mbili tofauti. Kama tuna upendo kwa MUNGU inatupasa sana kushirikiana na MUNGU na kuwasiliana na MUNGU Mara kwa Mara. Mawasiliano hayo ni maombi . Lakini maombi tu hayawezi kuzaa matunda kama sio maombi ya imani. Kama kuna mambo matano(5) muhimu katika maombi yako basi ni hivi: =Jina la YESU KRISTO(Yohana 14:14), =Damu ya YESU KRISTO(Ufunuo 12:11), = Neno la MUNGU la ufunuo wa ROHO MTAKATIFU(Zaburi 107:20), =Nguvu za ROHO MTAKATIFU(Luka 1:35a) =Na Kuomba kwa imani(Waebrania 11:6) --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Somo la sadaka kutoka kwa mtumishi wa Mungu Mwakasege --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
Somo la sadaka kutoka kwa Mwalimu Mwakasege --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message
KAZI KUU TANO (5) ZA IMANI KATIKA MAOMBI Uhusiano ni upendo unaozaa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande mbili tofauti. Kama tuna upendo kwa MUNGU inatupasa sana kushirikiana na MUNGU na kuwasiliana na MUNGU Mara kwa Mara. Mawasiliano hayo ni maombi . Lakini maombi tu hayawezi kuzaa matunda kama sio maombi ya imani. Kama kuna mambo matano(5) muhimu katika maombi yako basi ni hivi: =Jina la YESU KRISTO(Yohana 14:14), =Damu ya YESU KRISTO(Ufunuo 12:11), = Neno la MUNGU la ufunuo wa ROHO MTAKATIFU(Zaburi 107:20), =Nguvu za ROHO MTAKATIFU(Luka 1:35a) =Na Kuomba kwa imani(Waebrania 11:6) --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
38 Kisha baadhi ya waandishi wa sheria na Mafarisayo wakam wambia, “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” 39 Lakini yeye akawajibu, “Kizazi cha watu waovu na wasiowaami nifu hutafuta ishara; lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile ya nabii Yona. 40 Kwa maana kama vile Yona alivyokaa katika tumbo la nyangumi kwa muda wa siku tatu mchana na usiku, vivyo hivyo mimi Mwana wa Adamu nitakaa siku tatu, mchana na usiku ndani ya ardhi. 41 Siku ya hukumu watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu wakati Yona alipowahubiria, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona. 42 Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kukihukumu kizazi hiki; kwa kuwa yeye alisafiri kutoka miisho ya dunia ili akaisikilize hekima ya Sulemani; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.” --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
11 Yesu alipomaliza maelekezo haya kwa wafuasi wake kumi na wawili wa karibu, aliondoka mahali pale. Akaenda katika miji ya Galilaya kuwafundisha watu na kuwaeleza ujumbe wa Mungu. 2 Yohana alipokuwa gerezani, alisikia kuhusu mambo yaliyokuwa yanatokea; mambo ambayo Masihi angefanya. Hivyo akawatuma baadhi ya wafuasi wake kwa Yesu. 3 Wakamuuliza, “Wewe ni yule tuliyekuwa tunamngojea, au tumsubiri mwingine?” 4 Yesu akajibu, “Rudini mkamwambie Yohana yale mliyosikia na kuona: 5 Vipofu wanaona. Viwete wanatembea. Watu wenye magonjwa ya ngozi wanaponywa. Wasiyesikia wanasikia. Wafu wanafufuliwa. Na habari njema inahubiriwa kwa maskini. 6 Heri ni kwa wale wasio na shida kunikubali.” 7 Wafuasi wa Yohana walipoondoka, Yesu alianza kuongea na watu kuhusu Yohana. Alisema, “Ninyi watu mlikwenda jangwani kuona nini? Mtu aliye dhaifu, kama unyasi unaoyumbishwa na upepo? 8 Hakika, ni nini mlichotarajia kuona? Aliyevaa mavazi mazuri? Hakika si hivyo. Watu wote wanaovaa mavazi mazuri wanapatikana katika ikulu za wafalme. 9 Hivyo mlitoka kuona nini? Nabii? Ndiyo, Yohana ni nabii. Lakini ninawaambia, Yeye ni zaidi ya hilo. 10 Andiko hili liliandikwa kuhusu Yohana: ‘Sikiliza! Nitamtuma mjumbe mbele yako. Yeye ataandaa njia kwa ajili yako.’ 11 Ukweli ni kuwa Yohana Mbatizaji ni mkuu kuliko yeyote aliyewahi kuja katika ulimwengu huu. Lakini hata mtu asiye wa muhimu katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yohana. 12 Tangu wakati wa Yohana Mbatizaji ulipokuja mpaka sasa, Ufalme wa Mungu umekabiliwa na mashambulizi. Watu wenye nguvu wamejaribu kuudhibiti ufalme huu.[ a ] 13 Kabla ya Yohana kuja, Sheria ya Musa na manabii wote wamesema kuhusu mambo ambayo yangetokea. 14 Na ikiwa mnaamini waliyosema, basi Yohana ni Eliya. Ndiye waliyesema angekuja. 15 Ninyi watu mnaonisikia, sikilizeni! 16 Ninaweza kusema nini kuhusu watu wanaoishi leo? Watu siku ya leo ni kama watoto wanaokaa katika masoko. Kundi moja la watoto linaliambia kundi lingine, 17 ‘Tuliwapigia filimbi, lakini hamkucheza; tuliimba wimbo wa maziko, lakini hamkuhuzunika.’ 18 Kwa nini ninasema watu wako hivyo? Kwa sababu Yohana alikuja na hakula vyakula vya kawaida na kunywa divai, na watu walisema, ‘Ana pepo ndani yake.’ 19 Mwana wa Adamu amekuja akila na kunywa, na watu husema, ‘Mwangalie! Hula sana na kunywa divai nyingi. Ni rafiki wa wakusanya kodi na wenye dhambi wengine.’ Lakini hekima inaonesha kuwa sahihi kutokana na yale inayotenda.” --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
34 Msidhani kuwa nilikuja duniani kuleta amani. Sikuja kuleta amani. Nilikuja kuleta vita. 35 Nimekuja ili hili litokee: ‘Mwana atamgeuka baba yake. Binti atamgeuka mama yake. Binti mkwe atamgeuka mama mkwe wake. 36 Hata watu wa familia zenu watakuwa adui zenu.’ 37 Wale wanaowapenda baba zao au mama zao kuliko wanavyonipenda mimi hawana thamani kwangu. Na wale wanaowapenda wana wao au binti zao kuliko wanavyonipenda mimi hawastahili kuwa wafuasi wangu. 38 Wale ambao hawataupokea msalaba waliopewa wanaponifuata hawastahili kuwa wanafunzi wangu na kunifuata. 39 Wale wanaojaribu kuyatunza maisha waliyonayo, watayapoteza. Lakini wale wanaoyaacha maisha yao kwa ajili yangu watapata uzima halisi. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Kisha wanafunzi wa Yohane Mbatizaji walimwendea Yesu, wakamwuliza, “Sisi na Mafarisayo hufunga mara nyingi; mbona wanafunzi wako hawafungi?” 15Yesu akawajibu, “Je, walioalikwa harusini hutakiwa kuomboleza wakati bwana arusi yupo pamoja nao? La, hasha! Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipo watakapofunga. 16“Watu hawatii kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu. Maana kiraka hicho kitararua hilo vazi kuukuu, na pale palipokuwa pameraruka pataongezeka. 17Wala watu hawaweki divai mpya katika viriba vikuukuu. Wakifanya hivyo, viriba hupasuka na divai ikamwagika, navyo viriba vikaharibika. Ila, watu huweka divai mpya katika viriba vipya, na vyote viwili, viriba na divai, vikahifadhiwa salama.” --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Yesu anaamuru dhoruba itulie 23Yesu alipanda mashua, na wanafunzi wake wakaenda pamoja naye. 24Mara, dhoruba kali ikatokea ziwani, hata mawimbi yakaanza kuifunika mashua. Yesu lakini alikuwa amelala usingizi. 25Wanafunzi wakamwendea, wakamwamsha wakisema, “Bwana, tuokoe, tunaangamia!” 26Yesu akawaambia, “Enyi watu wenye imani haba; mbona mnaogopa?” Basi, akainuka, akaukemea upepo na lile ziwa; kukawa shwari kabisa. 27Watu wakashangaa, wakasema, “Ni mtu wa namna gani huyu? Hata pepo na bahari vinamtii!” Yesu anaponya watu wawili wenye pepo 28Yesu alifika katika nchi ya Wagadara, ngambo ya ziwa, na huko watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitokea makaburini. Watu hawa walikuwa wenye kutisha mno, hata hakuna mtu aliyethubutu kupita njia hiyo. 29Nao wakaanza kupiga kelele, “Una shauri gani nasi, wewe Mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya wakati wake?” 30Karibu na mahali hapo kulikuwa na nguruwe wengi wakichungwa. 31Basi, hao pepo wakamsihi, “Ikiwa utatutoa, basi uturuhusu tuwaingie nguruwe wale.” 32Yesu akawaambia, “Haya, nendeni.” Hapo wakawatoka watu hao, wakawaingia nguruwe. Kundi lote la nguruwe likaporomoka kwenye ule mteremko mkali, likatumbukia ziwani; nguruwe wote wakafa majini. 33Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakaenda mjini. Huko walitoa habari zote na mambo yaliyowapata wale watu waliokuwa wamepagawa. 34Basi, watu wote katika mji ule walitoka, wakamwendea Yesu; na walipomwona, wakamsihi aondoke katika nchi yao. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
“Msiwahukumu wengine, msije nanyi mkahukumiwa na Mungu; 2kwa maana jinsi mnavyowahukumu wengine, ndivyo nanyi mtakavyohukumiwa; na kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho Mungu atakachotumia kwenu. 3Kwa nini wakiona kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako? 4Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ wakati wewe mwenyewe unayo boriti jichoni mwako? 5Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyomo jichoni mwako na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako. 6“Msiwape mbwa vitu vitakatifu wasije wakageuka na kuwararua nyinyi; wala msiwatupie nguruwe lulu zenu wasije wakazikanyaga. 7“Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni mlango, nanyi mtafunguliwa. 8Maana, yeyote aombaye hupewa, atafutaye hupata, na abishaye mlango hufunguliwa. 9Je, kuna yeyote miongoni mwenu ambaye mtoto wake akimwomba mkate, atampa jiwe? 10Au je, akimwomba samaki, atampa nyoka? 11Kama basi nyinyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: Atawapa mema wale wanaomwomba. 12“Yote mnayotaka watu wawatendee nyinyi, watendeeni wao vivyo hivyo. Hii ndiyo maana ya sheria ya Mose na mafundisho ya manabii. 13“Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba. Kwa maana njia inayoongoza kwenye maangamizi ni pana, na mlango wa kuingilia humo ni mpana; waendao njia hiyo ni wengi. 14Lakini njia inayoongoza kwenye uhai ni nyembamba, na mlango wa kuingilia humo ni mwembamba; ni watu wachache tu wanaoweza kuigundua njia hiyo. Mti hujulikana kwa matunda yake 15“Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo kwa nje, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali. 16Mtawatambua kwa matendo yao. Je, watu huchuma zabibu katika miti ya miiba, au tini katika mbigili? La! 17Basi, mti mzuri huzaa matunda mazuri, na mti mbaya huzaa matunda mabaya. 18Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19Kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni. 20Kwa hiyo, mtawatambua kwa matendo yao. --- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message…
Добро пожаловать в Player FM!
Player FM сканирует Интернет в поисках высококачественных подкастов, чтобы вы могли наслаждаться ими прямо сейчас. Это лучшее приложение для подкастов, которое работает на Android, iPhone и веб-странице. Зарегистрируйтесь, чтобы синхронизировать подписки на разных устройствах.