Работайте офлайн с приложением Player FM !
Droo ya CHAN 2024: Kenya yapangwa kundi gumu zaidi, mashindano ya Agosti 2025
Manage episode 461803647 series 1197326
Kipindi cha leo kimeangazia pakubwa droo ya mashindano ya CHAN 2024; adhari ya kuahirishwa kwa kipute na uchambuzi wa makundi. Pia tumetupia jicho raundi ya sita hatua ya makundi mechi za klabu bingwa Afrika, fainali ya mashindano mapya ya wasichana U17, Shujaa yataja kikosi chake cha mkondo wa Perth 7s, Kipchoge akilenga taji la tano la London Marathon, Tyson Fury astaafu ndondi kwa mara ya pili pamoja na mashindano ya tenisi ya Australian Open yakiingia hatua ya robo fainali.
Kulingana na droo iliyofanyika Jumatano usiku katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi nchini Kenya, Harambee Stars imepangwa katika 'kundi la kifo' ambapo itamenyana na mabingwa mara mbili Morocco (2018 na 2020) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (2009 na 2016).
"Tuko kwenye kundi la kifo," Mariga alikiri, akibainisha uimara wa wapinzani wao.
"Hizo ni timu kubwa na inamaanisha lazima tuweke juhudi zaidi katika maandalizi."
“Wapinzani wetu ni wagumu, tutashiriki mashindano haya kwa mara ya kwanza lakini haijalishi. Tuna wachezaji wazuri ambao wanaweza kutoa changamoto,” alijibu Kenneth Muguna, mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi cha sasa cha Harambee Stars.
Pia katika Kundi A kuna Zambia na Angola. Kenya itakuwa mwenyeji wa mashindano haya yanayofanyika kila baada ya miaka miwili kwa wachezaji wa nyumbani pamoja na Tanzania na Uganda.
Wenyeji wenza Tanzania wako katika Kundi B ambapo watamenyana na Madagascar, Mauritania, Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
“Tusichukulie kundi hili kama jepesi, sisi kama wenyeji lazima tujitayarishe vyema ili tupite awamu ya makundi na hata kushinda kombe, “ alisema rais wa shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) Wallace Karia.
Uganda wataongoza Kundi C ambapo watamenyana na Niger na nchi mbili ambazo zitatinga hatua ya mwisho ya mchujo. Mabingwa watetezi Senegal wataanzisha tena uhasama na Nigeria katika kundi D, ambayo pia ina Sudan na Kongo.
“Tumecheza dhidi ya Guinea na Niger mara kadhaa, tunajua wanavyocheza. Tumefuzu mara ya nane mashindano haya, na hatujawahi kuaga mashindano kwenye makundi,” alieleza kwa msisimko Moses Magogo, rais wa shirikisho la soka (FUFA) nchini Uganda.
Michuano hiyo yenye timu 19 ambayo awali ilipangwa kufanyika Februari 1 hadi 28, iliahirishwa hadi Agosti mwaka huu. Wasaidizi wa droo hiyo walikuwa wachezaji wa zamani - McDonald Mariga wa Kenya, Mrisho Ngasa wa Tanzania na Hassan Wasswa wa Uganda huku mkurugenzi wa mashindano wa CAF, Samson Adamu akisimamia mchakato wa droo.
Katika ujumbe wake wa video kabla ya droo hiyo, rais wa CAF Patrice Motsepe alitoa shukrani zake kwa marais William Ruto (Kenya), Samia Suluhu Hassan (Tanzania) na Yoweri Museveni (Uganda) kwa ushirikiano wao kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa mafanikio.
"Ukarabati wa viwanja, viwanja vya kufanyia mazoezi, miundombinu, hoteli na hospitali katika nchi hizo tatu unaonyesha maendeleo makubwa na motisha, iliyodhihirika wakati wa ziara yangu," ujumbe wake Motsepe ulibainisha.
"Lengo lilikuwa kuunganisha mataifa matatu ya Afrika Mashariki, pamoja na mengine kutoka sehemu mbalimbali za Afrika."
Waziri wa Michezo nchini Kenya Salim Mvurya alipamba hafla hiyo pamoja na wenzake kutoka Uganda na Tanzania, Peter Ogwang na profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko.
Droo Kamili
Kundi A: Kenya, Morocco, Angola, DR Kongo, Zambia
Kundi B: Tanzania, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso, Jamhuri ya Afrika ya Kati
Kundi C: Uganda, Niger, Guinea, Q2, Q1
Kundi D: Senegal, Kongo, Sudan, Nigeria
24 эпизодов

Все серии
×Добро пожаловать в Player FM!
Player FM сканирует Интернет в поисках высококачественных подкастов, чтобы вы могли наслаждаться ими прямо сейчас. Это лучшее приложение для подкастов, которое работает на Android, iPhone и веб-странице. Зарегистрируйтесь, чтобы синхронизировать подписки на разных устройствах.